Jina ''Tor'' inaweza kurejea vifaa kadhaa tofauti.
Tor ni programu unayoweza kuendesha katika kompyuta yako ambayo inakusaidia kuwa salama katika mtandao.
Inakulinda wewe kwa kukukwepesha mawasiliano yako katika relay za mtandao uliosambazwa kwa watu wote wanaojitolea duniani: inazuia mtu kuona muunganiko wa mtandao wako kwa kutazama tovuti zipi umezitembelea, na inazuia kugundua tovuti ulizotembelea kutoka kwenye eneo lako halisi ulilopo.
Mkusanyiko huu wa kujitolea unaitwa Mtandao wa Tor.
Namna watu wengi hutumia Tor pamoja na Tor Browser, ambayo ni toleo la Firefox ambayo hurekebisha mambo ya faragha.
Unaweza kusoma zaidi kuhusu Tor kwenye kurasa yetu ya kuhusu.
Tor Project ni taasisi isiyoingiza faida (msaada) ambayo inadumisha na kuendeleza programu ya Tor.