Misc

Tunasikikita sana, kwamba umeathirika na programu hasidi. Tor Project haijatengeneza malware hii. Watengenezaji wa malware wanakutafuta upakue Tor Browser labda uwatafute wao bila kujulikana kwa fidia ambayo wanaitaka kutoka kwako.

Kama hii ndo mara yako ya kwanza kutumia Tor Browser, tunaelewa kuwa unaweza kudhani ni watu wabaya ambao tunawawezesha watu wabaya pia.

Lakini zingatia programu yetu hutumika kila siku kwa malengo mengi ya wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari, waathirika wa unyanyasaji wa majumbani, watoa taarifa, maafisa utekelezaji wa sheria, na wengine wengi. Kwa bahati mbaya udhibiti ambao programu yetu unaweza kutoa kwa makundi haya ya watu unaweza pia kutumiwa vibaya na wahalifu na watengenezaji programu hatarishi. Tor Project haisaidii au kusamehe utumiaji wa programu yetu kwa lengo la kuhasidi.

Sasa hivi urefu wa njia umepangiwa kwa nguvu katika 3 zaidi ya idadi ya nodi katika njia yako ambayo ni nyeti. Kwa kawaida, ni 3 katika hali za kawaida, lakini kwa mfano, ikiwa unatumia onion service au anwani ya ".exit" inaweza kuwa zaidi.

Hatutaki kuhamasisha watu kutumia njia ndefu zaidi ya hii kwa sababu inaongeza mzigo kwenye mtandao bila kutoa ulinzi wowote (kadri tunavyoweza kuona. Pia, kutumia njia ndefu zaidi ya tatu kunaweza kudhuru utambulisho wako usiojulikana, kwanza kwa sababu inafanya mashambulizi ya kukanusha usalama kuwa rahisina pili kwa sababu inaweza kutumika kama kitambulisho ikiwa idadi ndogo tu ya watumiaji wana urefu wa njia sawa na wewe.

Hakuna ambacho watengenezaji wa Tor wanaweza kufanya kufuatilia watumiaji wa Tor. Ulinzi sawa unaowazuia watu wabaya katika kuharibu kutokujulikana kwa Tor's pia hutulinda katika kuchukua taarifa za mtumiaji.

hapana, Tor project hawezi kutoa huduma za uendeshaji.

Tor imeundwa kutetea haki za binadamu na faragha kwa kuzuia mtu yeyote kudhibiti vitu, hata sisi. Tunachukia kuwa kuna baadhi ya watu ambao hutumia Tor kufanya mambo ya kutisha, lakini hatuwezi kufanya kitu chochote ili tuwaondoe katika hilo bila ya kudhohofisha wanaharakati wa haki za binadamu, unyanyasaji wa manusura, na watu wengine amabao hutumia Tor kwa mambo mazuri. Kama tunataka kuzuia baadhi ya watu kutumia Tor, tutaongeza mlango wa dharula katika programu, ambao utafunguka kwa watumiaji wetu ambao wapo katika hatari ya kushambuliwa na utawala mbaya na wapinzani.

Tor inategemea msaada wa watumiaji na wajitoleaji ulimwenguni kote kutusaidia kuboresha programu yetu na rasilimali, kwa hivyo maoni yako ni muhimu sana kwetu (na kwa watumiaji wote wa Tor).

fomu ya mrejesho

wakati Unatutumia maoni au kutoa taarifa kuhusu hitilafu, tafadhali jumuisha na vingine iwezekanavyo:

  • mfumo wa uendeshaji unaotumia
  • Toleo la Tor Browser
  • Kiwango cha ulinzi wa Tor Browser
  • Hatua kwa hatua jinsi ya kupata suala hilo, ili unaweza kulizalisha tena (kwa mfano Nimefungua kivinjari, nikaandika url, nikabofya (i) icon, kisha kivinjari changu kikapotea)
  • skrini yenye tatizo
  • kumbukumbu

namna ya kutufikia

Kuna njia mbalimbali za kuwasiliana nasi,tafadhali chagua ipi itakufaa zaidi.

jukwaa la Tor

Tunashauri kuomba msaada katika Jukwaa laTor. Utahitaji kutengeneza akaunti ili kuwasilisha mada mpya. Kabla hujauliza, tafadhari hakiki miongozo yetu ya majadiliano. Kwasasa, kwa majibu ya mwisho, tafadhali andika kwa kingereza. Ikiwa umepata programu iliyoharibika, tafadhari tumia GitLab.

#### Gitlab

Kwanza, angalia kama tatizo limejulikana. Unaweza kutafuta na kusoma matatizo katika https://gitlab.torproject.org/. Kuunda jambo jipya, tafadhaliomba akaunti mpya kuipata Tor Project's GitLab haraka na tafuta hifadhi sahihi kutoa taarifa ya tatizo. Tunafuatilia matatizo yote yahusianayo na Tor Browser Tor Browser issue tracker. Matatizo yahusianayo na tovuti yetu yanatakiwa kujazwa katika Kinasa matatizo ya tovuti.

Telegram

Ikiwa unahitaji kusanikisha au troubleshooting Tor Browser na Tor Forum ikizuiliwa au kudhibitiwa mahali ilipo, unaweza kutufikia katika Telegram https://t.me/TorProjectSupportBot. Mtaalam wa msaada wa Tor atakusaidia.

whatsApp

Unaweza kuwasiliana na nasi kwa kutuma ujumbe wa maandishi katika namba yetu ya WhatsApp: +447421000612. Huduma hii inapatikana tu kwa ujumbe wa mandishi; video au simu hazijawezeshwa.

signal

Unaweza kupata msaada kwa kutuma ujumbe wa maandishi katika namba yetu ya Signal: +17787431312. Signalni programu ya matumizi ya bure na imelenga ufaaragha kwa watumiaji. Huduma hii inapatikana tu kwa ujumbe wa mandishi; video au simu hazijawezeshwa. Baada ya kutuma ujumbe,watu wetu wa msaada watakusaidia kutatua tatizo.

barua pepe

Send us an email to frontdesk@torproject.org.

Katika kichwa cha habari cha barua pepe yako, tafadhali tujulishe unatoa taarifa ya kitu gani. Namna ambavyo kichwa cha habari cha barua pepe kinakuwa mahususi mfano. "Kushindwa kuunganishwa", "mrejesho katika tovuti", "Mrejesho katika Tor Browser, "Nahitaji bridge"), ndivyo itakavyokuwa rahisi kwetu kuelewa na kufuatilia. Wakati mwingine tunapopokea barua pepe zisizo na kichwa cha habari,huingia katika barua pepe zisizothibitishwa na tunashindwa kuziona.

Kwa majibu ya haraka, tafadhari andika kwa Kiingereza, Kihispania, na/au Kireno ikiwa unaweza. Kama hakuna lugha unayoielewa kati ya hizi, tafadhali andika kwa lugha yoyote unayoweza, lakini jua kwamba muda kidogo kujibu sababu tutahitaji msaada wa kutafsiriwa ili kuelewa.

blog ya kuweka maoni

Unaweza kuacha maoni kwenye chapisho la blogu linalohusiana na suala au mrejesho unayotaka kutolea taarifa. Ikiwa hakuna chapisho katika suala lako, tafadhari wasiliana nasi kwa njia ingine.

IRC

Unaweza kutupata kupitia #tor kwenye OFTC ili kutupatia maoni au kuripoti makosa. Hatujibu mara moja, lakini tunachunguza orodha ya kazi zilizobaki na tutakujibu kadri tunavyoweza.

Jifunze jinsi ya kujiunga katika OFTC servers.

orodha ya barua pepe

Kwa kutoa ripoti masuala au majibu ya kutumia orodha ya barua pepe, tunapendekeza kwamba ufanye hivyo kwa ile inayohusiana na kile ambacho ungependa kuripoti. Saraka iliyokamilika katika orodha yetu ya barua pepe inaweza kupatikana hapa.

Kwa majibu au masuala yanayohusiana na tovuti yetu: ux

Kwa mrejesho na masuala yahusuyo kutumia Tor relay: tor-relays

toa taarifa ya kiusalama

Ikiwa umepata suala la kiusalama, tafadhari tutumie barua pepe security@torproject.org.

Ikiwa unataka kusimba barua pepe yako, unaweza kupata funguo la umma ya OpenPGP kwa anwani hii kutoka keys.openpgp.org. Here is the current fingerprint:

  pub   rsa3072/0x3EF9EF996604DE41 2022-11-15 [SC] [expires: 2024-12-11]
      Key fingerprint = 835B 4E04 F6F7 4211 04C4  751A 3EF9 EF99 6604 DE41
  uid Tor Security Contact <security@torproject.org>
  sub   rsa3072/0xF59EF1669B798C36 2022-11-15 [E] [expires: 2024-12-11]
      Key fingerprint = A16B 0707 8A47 E0E1 E5B2  8879 F59E F166 9B79 8C36

Ikiwa unapenda kushiriki katika programu yetu ya bug bounty, tafadhari kuwa makini, kuwasilisha suala la usalama katika tovuti ya watu wengine hubeba hatari fulani ambayo hatuwezi kuidhibiti, ndio matokeo tunapendelea kuripoti moja kwa moja.

Hata kama maombi yako yanatumia toleo sahihi la itifaki ya SOCKS, bado kuna hatari kwamba inaweza kuvuja maswali ya DNS. Tatizo hili hutokea kwenye vipengele vya Firefox ambavyo hupata majina ya kikoa ya marudio wenyewe, kwa mfano kuonyesha anwani yake ya IP, nchi ilipo, n.k. Ikiwa una mashaka kwamba programu yako inaweza kujitokeza hivi, fuata maelekezo hapo chini ili uweze kufanya uchunguzi.

1.ongezaTestSocks 1kwenyetorrc fileyako. Anza Tor, na weka mipangilio ya proksi ya programu yako kuwa kwenye seva ya SOCKS5 ya Tor (socks5://127.0.0.1:9050 kwa chaguo-msingi). 1 Angalia kumbukumbu zako unapotumia programu yako. Kwa kila uunganisho wa soksi, Tor itarekodi onyo kwa uunganisho salama, na onyo la tahadhari" kwa uunganisho unaovuja maombi ya DNS.

Ikiwa unataka kuzima moja kwa moja uunganisho wote unaovuja maombi ya DNS, weka SafeSocks 1 katika faili yako ya torrc.

Ahsante kwa ushirikiano wako! Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu kuchangia mradi wetu FAQ.

kwa kushea faili kupitia Tor, OnionShare ni chaguo zuri. Onion share ni nyenzo huru kwa ajili ya ulinzi na kutojulikana wakati wa kutuma na kupokea mafaili unapotumia Tor onion services. Inafanya kazi kwa kuanzisha seva ya wavuti moja kwa moja kwenye kompyuta yako na kuitengeneza kama anwani ya wavuti ya Tor isiyoweza kubashiriwa ambayo wengine wanaweza kuitumia kwenye Tor Browser kupakua faili kutoka kwako, au kupakia faili kwako. Haihitaji kuweka seva tofauti, kutumia huduma ya kushirikisha faili ya watumiaji wasio wa moja kwa moja au hata kuingia kwenye akaunti.

Tofauti na huduma kama email, Google Drive, DropBox, WeTransfer, au njia nyingine ambayo watu hutuma mafaili kwa kila mtu, unapoona onion share haujatoa ruhusa ya mafaili ambayo umeyasambaza. Ili mradi unasambaza anwani ya tovuti isiyowezekana kwa njia iliyo salama (kama kunakirisha katika programu ya ujumbe iliyosimbwa) hakuna mtu isipokuwa wewe na mtu uliyesambazia mafaili.

Onion Share imetengenezwa na Micah Lee.

Exit node nyingi zimesanidiwa kuzuia aina fulani za usafirishaji wa mafaili, kama vile BitTorrent. Hususan BitTorrent haifanyi kwa siri kupitia Tor.

Hapana. Baada ya toleo la kumi na moja la beta, hatujaendelea na msaada wa Tor Messenger. Bado tunaamini katika uwezo wa Tor kutumika katika programu za ujumbe, lakini hatuna rasilimali kuwezesha hilo kwa sasa. Je wewe? wasiliana nasi.

Vidalia hayupo tena katika kudumisha wala usaidizi. Sehemu kubwa ya vipengele vya Viladia sasa imejumuishwa na Tor Browser.

Tor inafadhiliwa na idadi ya wafadhili tofauti ikiwemo mashirika ya shirikisho ya US, taasisi binafsi, na wafadhili binafsi. Tazama orodha ya wafadhili wetu na mfululizo wa blog posts kwenye ripoti zetu za fedha.

Tunapenda kuwa wawazi kuhusu wafadhili wetu na namna ya ufadhili ni namna bora ya kuboresha uaminiu katika jamii yetu. Siku zote tunatafuta uwanda mpana wa rasilimali, hususani kutoka kwenye taasisi na watu binafsi.

Vitu vichache ambavyo kila mtu anweza kufanya sasa:

  1. Tafadhali zingatia kutumia relay kusaidia kukuza mtandao wa Tor.
  2. Waambie marafiki zako! Watumie relay. Wafanye watumie onion services. Waambie wawaambie marafiki zao. 1.Kama unapenda malengo ya Tor, tafadhali chukua muda kuchangia kusaidia maendeleo zaidi ya Tor. Pia tunatafuta wafadhili zaidi-kama unazijua kampuni zozote, NGOs, mashirika, au taasisi nyingine zozote ambazo zinataka faragha/ usalama wa mawasiliano, wafahamishe kuhusu sisi.
  3. Tunatafuta mifano mizuri zaidi ya watumiaji wa Tor na kesi za matumizi ya Tor. Kama unatumia Tor kwa mazingira au lengo ambalo halijaelezewa katika ukurasa huo, na utakua huru kusambaza kwetu, tutapenda kusikia kutoka kwako.

Nyaraka

  1. Saidia localize uwasilishaji katika lugha nyingine. Tazama kuwa mtafsiri wa Tor kama unataka kutusaidia. Tunahitaji tafsiri ya Kiarabu au Farsi, kwa watumiaji wengi ya Tor katika maeneo ya udhibiti.

Utetezi

1.Jumuiya ya Tor hutumia jukwaa la Tor, IRC/Matrix, na public mailing lists.

  1. Tengeneza maelezo ambayo yanaweza kutumika kwa watumiaji wengi mikutano ya kikundi duniani kote.
  2. Tegeneza bango kuhusu dhima, kama vile "Tor kwa haki za binadamu!".
  3. Sambaza ulimwenguni kuhusu Tor katika mikusanyiko au mikutano na utumie vipeperushi hivi vya Tor kama chanzo ya mazungumzo.

kuna sababu chache ambazo hatuzifanyi:

Hatuwezi kusaidia lakini kuifanya habari ipatikane, kwani wateja wa Tor wanahitaji kuitumia kuichagua njia yao. Ikiwa hivyo, iwapo "wazuiaji" wanataka hiyo, wanaweza kuipata kwa njia yoyote. Zaidi ya hayo, hata kama hatukuwaambia watumiaji kuhusu orodha ya njia za usambazaji moja kwa moja, bado mtu anaweza kufanya uhusiano mwingi kupitia Tor kwenda kwenye tovuti ya majaribio na kujenga orodha ya anwani wanazoziona. Ikiwa watu wanataka kutuzuia, wanaamini wanapaswa kuruhusiwa kufanya hivyo. Dhahiri, tungeweza kupendelea kila mtu kuruhusu watumiaji wa Tor kuungana nao, lakini watu wana haki ya kuamua ni nani anayestahili kuunganisha kwenye huduma zao, na ikiwa wanataka kuzuia watumiaji wasiojulikana, wanaweza kufanya hivyo.

  1. Kuweza kuzuiliwa pia kuna faida za kimkakati: inaweza kuwa jibu la kushawishi kwa wamiliki wa tovuti ambao wanahisi kudhulumiwa na Tor. Kuwapa chaguo kunaweza kuwahamasisha kusimama na kufikiria iwapo wanataka kweli kufuta ufikiaji binafsi kwenye mfumo wao, na ikiwa sivyo, chaguo zingine wanazoweza kuwa nazo. Wakati ambao wangeweza kutumia kuzuia Tor, badala yake wanaweza kutumia muda huo kufikiria upya mtazamo wao kwa uhuru na kutokuonekana kwa jumla.

Tor haijahifadhi log zozote ambazo zinaweza zikamtambua mtumiaji husika. Tumezingatia vipimo salama vya namna ya ufanyaji kazi wa mtandao, ambazo unaweza ukatazama kwenye Vipimo vya Tor.

Kuhusu Kuhifadhi kumbukumbu Habari Kazi Blogi Jarida Mawasiliano Changia Msaada jumuiya Maswali yanayoulizwa sana Kuhusu Tor Tor Browser Tor Messenger Tor-rununu GetTor Tor Inaunganishwa Udhibiti HTTPS mafundi OnionServices Hifadhi ya Debian Hifadhi ya RPM ubunifu mwingine little-t-tor Misc abuse FAQs Wasiliana