OnionServices

Nawezaje kujua kama natumia onion service za v2 au v3?

Unaweza kutambua teleo la 3 la anwani ya onion kwa urefu wa herufi 56, mfano. Tor Project's v2 address:http://expyuzz4wqqyqhjn.onion/, and Tor Project's v3 address: http://2gzyxa5ihm7nsggfxnu52rck2vv4rvmdlkiu3zzui5du4xyclen53wid.onion/

Ikiwa wewe ni msimamizi wa onion service, unapaswa kusasisha toleo la 3 la onion service haraka iwezekanavyo. Ikiwa wewe ni mtumiaji, tafadhari hakikisha umesasisha alamisho yako katika anwani ya tovuti toleo la 3 la onion.

Rekodi yako ya matukio ni ipi kwenye v2?

Mnamo September 2020, Tor walianza kutoa onyo kwa waendeshaji na watumiaji wa onion service kuwa toleo la 2 litaacha kutumika na toleo la zamani la 0.4.6. Tor Browser ilianza kutoa onyo kwa watumiaji wake June, 2021.

MnamoJuly 2021, toleo la 0.4.6 la Tor haitatumia tena toleo la 2 na usaidizi utaondolewa katika msingi wa msimbo.

Mnamo October 2021, Tutatoa toleo jipya la watumiaji wa Tor toleo lililo imara kwa safu zote ambazo zitaondoa uwezo wa toleo la 2.

Unaweza kusoma zaidi katika machapisho ya blog ya Tor project's Onion Service version 2 deprecation timeline.

Ninaweza kuendelea kutumia anwani za onion zangu za v2? Ninaweza kupata onion zangu za v2 baada ya mwezi wa tisa? Hii ni mabadiliko ya nyuma yasiyolingana?

Anwani za toleo la 2 la onion hazipo salama kimsingi, Kama una toleo la 2 la onion, tunapendekeza uache kulitumia. Haya ni mabadiliko ya awali yasiyoendana: Toleo la 2 la onion services haitapatika baada ya September 2021.

Ni pendekezo gani kwa watengenezaji programu ili kuhamisha? Vidokezo vyovyote vya namna ya kusambaza anwani mpya za V3 kwa watu?

Katika torrc, kutengeneza anwani ya toleo la 3, utahitaji tu kuanzisha huduma mpya kama ulivyofanya tu katika huduma ya toleo la 2, kupitia mistari hii miwili:

HiddenServiceDir /full/path/to/your/new/v3/directory/
HiddenServicePort <virtual port> <target-address>:<target-port>

Toleo lililozoeleka kwa sasa limepangiliwa kuwa la 3 kwa hivyo hupaswi kuweka wazi. Anzisha tena tor, na angalia katika saraka yako kwa ajili ya anwani mpya. Ikiwa unataka kuendelea kutumia huduma yako ya toleo la 2 hadi pale itakapoacha kutoa njia ya mpito kwa watumiaji wako, ongeza mstari huu ili kusanidi huduma yako ya toleo la 2 iliyozuiliwa:

HiddenServiceVersion 2

Hii itakuruhusu kutambua faili lako ulilolisanidi ni lipi katika toleo lipi.

Ikiwa una Onion-Location sanikisha tovuti yako, unahitaji kupangilia kichwa cha habari na toleo lako la 3 jipya la anwani. Kwa nyaraka ya kiufundi kuhusu kutumia onion services, tafadhari soma kurasa ya Onion Services katika Portal yetu ya kijamii.

Sijaona tangazo, ninaweza kupata muda zaidi wa kuhama?

Hapana, mawasiliano ya toleo la 2 yataanza kushindwa sasa hivi, kuanza polepole, kisha ghafla. Ni wakati wa kuyaondoka.

Huduma zitaanza kushindwa kufika mwezi wa tisa, au tayari kabla?

Tayari, alama za utangulizi hazipo katika Tor 0.4.6 kabisa, hivyo haziwezi kupatikana kama waendesha relay watasasisha.

Wasimamizi wa tovuti, ninaweza kurudia kuwaongoza watumiaji kutoka kwenye onion ya v2 hadi v3?

Ndio, Itafanya kazi hadi toleo la 2 la onion address lisipopatikana. Unaweza kuhitaji kuwahimiza watumiaji kusasisha amalisho zao.

Onion service za v3 inakwenda kusaidia kupunguza matatizo ya DDoS?

Ndio, tunaendelea kushughulikia katika kuboresha usalama wa onion services. Baadhi ya kazi tulizonazo katika mipango yetu ni ESTABLISH_INTRO Cell DoS Defense Extension, Res tokens: Anonymous Credentials for Onion Service DoS Resilience, na A First Take at PoW Over Introduction Circuits. Kwa muhtasari kuhusu mapendekezo haya, soma chapisho la blog Namna ya kuzuia kushindwa kwa onion (za huduma).

Onion-Location ni HTTP header mpya ambazo tovuti zinaweza kutumia kutangaza onion mwenzao. Ikiwa tovuti unayoitembelea ina tovuti ya onion inayopatikana, taarifa ya pendekezo la zambarau itaonekana katika sehemu ya kuandikia anwani ikisema ".onion available". Ukibofya katika ".onion available",tovuti itatafuta data tena na kukupeleka katika onion zingine. Kwa sasa, Onion-Location inapatikana katika Tor Browser ya kompyuta ya mezani (Windows, macOS na GNU/Linux). Unaweza kujifunza zaidi kuhusu Onion-Location katika Mpangilio wa Tor Browser. Ikiwa wewe ni muendeshaji wa onion service, jifunze jinsi ya kusanidi Onion-Location katika tovuti yako ya onion.

Onion Service iliyothibitishwa ni onion service inayohitaji kukupatia tokeni za uthibitishaji (kwa suala hili, funguo binafsi) kabla ya kufikia huduma. Funguo binafsi huwa haisambazwi katika huduma, na husimba kifafanuzi chake pekee cha ndani ya nchi. Unaweza kupata vitambulisho vya ufikiwaji kutoka kwa muendeshaji wa onion service, Kuwafikia waendeshaji na maombi ya ufikiwaji. Jifunze zaidi kuhusu jinsi ya kutumia uthibitishaji wa onion katika Tor Browser. If you want to create an onion service with client authentication, please see the Client Authorization in the Community portal.

Unapo peruzi Onion Service, Tor Browser huonyesha aina tofauti za alama za onion kwenye anwani ya bar ikionyesha ulinzi wa ukurasa wa tovuti wa sasa.

Picha ya onion Onion inamaanisha:

  • Onion Services inatolewa na HTTP, au HTTPS ikiwa na cheti ya CA.
  • Onion Services inatolewa na HTTPS na cheti kilichosainiwa chenyewe.

Picha ya onion ikiwa na mkwaju mwekundu Onion ikiwa na mkwaju mwekundu humaanisha:

  • Onion Service hutolewa na muongozo kutoka kwenye URL isiyo na ulinzi.

Picha ya onion ikiwa na alama ya tahadhari Onion ikiwa na alama ya tahadhari humaanisha:

  • Onion Service hutolewa na HTTPS ikiwa na cheti kilichoisha muda wake.
  • Onion Service inatolewa na HTTPS katika kikoa kisicho sahihi.
  • Onion Service hutolewa na mchanganyiko wa URL isiyo salama.

Tovuti ambazo zinafikiwa katika Tor pekee zinaitwa "onions" na mwishoni mwa TLD .onion. Kwa mfano, DuckDuckGo onion ni https://duckduckgogg42xjoc72x3sjasowoarfbgcmvfimaftt6twagswzczad.onion/. Unaweza kuzifikia tovuti hizi kwa kutumia Tor Browser. Anwani inapaswa kusambazwa kwako na mmiliki wa tovuti, kama onion na sio kielezo katika kitafutaji kwa njia za kawaida ambazo tovuti za vanilla zipo.

Kama huwezi kuipata onion services unazo taka, hakikisha umeingiza onion address 56 kwa usahihi; hata makosa madogo itazuia Tor Browser ili uweze kuzifikia site. Kama bado una shindwa kujiunga na onion services, tafadhali jaribu tena baadaye. Inaweza kuwa na tatizo la muda mfupi la muunganiko, au wanaoendesha tovuti wanaweza kuwa wameruhusu kukatika kwa mtandao bila angalizo.

Pia unaweza kuhakikisha kuwa unaweza kuzipata onion services kwa kujiunga na onion services za DuckDuck.

Onion services huruhusu watu kuvinjari lakini pia kuchapisha kutokujulikana, ikiwemo kuchapisha tovuti zisizojulikana.

Onion services pia hutegemewa kwa mawasiliano ya data ya metadata na usambazaji wa faili, mwingiliano salama kati ya waandishi wa habari na vyanzo kama vile SecureDrop au OnionShare, kusasisha salama programu, na njia salama zaidi za kufikia tovuti maarufu kama Facebook.

Huduma hizi hutumia matumizi maalumu ya kiwango cha juu cha kikoa (TLD) .onion (badala ya .com, .net, .org n.k) na zinapatikana kwa njia ya mtandao wa Tor pekee.

Nembo ya Onion

Unapotumia tovuti inayotumia onion service, Tor Browseritaonyesha katika sehemu ya kuandika URL alama ya onion itaonyesha hali ya mawasiliano yako: salama na kutumia onion service.

Kujifunza zaidi kuhusu onion services, soma Jinsi Onion Service zinavyofanya kazi?